<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><lyrics>[V1]
 1. Mwamba uliopasuka, ndani yako nijifiche! Maji yale, damu ile itokayo mbavu zako, iwe dawa ya kuponya roho yangu na ubaya!

[V2]
 2. Kazi za mikono yangu, haziwezi kukomboa. Hata ningelia sana na kutenda kazi nyingi, singeweza kuokoka, peke yako u Mwokozi.

[V3]
 3. Ndani yangu sina kitu, naushika msalaba. Uchi mimi, univike! Sina nguvu, nichukue! Ni mchafu, unioshe! Wewe u Mwokozi wangu.

[V4]
 4. Kwa maisha yangu yote hata nitatoa roho, hata saa ya kuitwa mbele ya Mfalme wangu, mwamba uliopasuka, nijifiche ndani yako!</lyrics>
<title>Mwamba uliopasuka</title>
</song>